Wananchi Manyara epukeni vishoka wa umeme
6 August 2024, 5:44 pm
Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji(Ewura) imewataka wananchi mkoani Manyara kuepuka vishoka ambao wamekuwa wakifanya kazi na kusababisha madhara makubwa kwenye mifumo ya umeme
Na Mzidalfa Zaid
Wananchi mkoani Manyara na kanda ya kaskazini kwa ujumla wametakiwa kutumia mafundi umeme ambao wamesajiliwa na wanye leseni Ili kuepuka vishoka ambao wamekuwa wakifanya kazi na kusababisha madhara makubwa kwenye mifumo ya umeme.
Wito huo umetolewa leo na afisa mahusiano na mawasiliano kutoka mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji(Ewura) Pamela Pallangyo alipokuwa akiongea na Fm Manyara amesema kuna baadhi ya mafundi umeme wanafanya kazi bila leseni.
Pallangyo amewataka wananchi kufika kwenye ofisi za Ewura pindi wanapohitaji ufafanuzi au wanapokutana na changamoto kuhusu sekta ya maji, umeme na gesi ili malalamiko yao yatatuliwe kwa urahisi..
Aidha, amesema kwa fundi yeyote ambae anahitaji kupata leseni afatilie kwenye mamlaka hiyo ili apatiwe leseni na afanye kazi kwa uhuru ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria na mamlaka husika.