FM Manyara

Gekul azungumza kwa mara ya kwanza, aeleza ilivyokuwa

1 December 2024, 9:21 pm

Mbunge wa jimbo la Babati Mjini mkoani Manyara kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Pauline Philipo leo amezungumza na wananchi wa jimbo la Babati mjini pamoja na vyombo vya habari baada ya kumshukuru mungu kwa mapitio aliyoyapitia

Na Mzidalfa Zaid

Mbunge wa jimbo la Babati Mjini mkoani Manyara kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Pauline Philipo leo amezungumza na wananchi wa jimbo la Babati mjini pamoja na vyombo vya habari baada ya kumshukuru mungu kwa mapitio aliyoyapitia ya kutuhumiwa kufanya vitendo vya ukatili.

Gekul amesema anamshukuru mungu kwa kuwa tukio alilotuhumiwa halikuwa la ukweli kwa kuwa cheti cha daktari kilithibitisha kuwa kijana Hashimu Ally aliyedai kuwa amemfanyiwa vitendo vya udhalilishaji hajafanyiwa hivyo kama ambavyo alikuwa akidai.

Amesema ametoa shukrani hizo kwa mungu lengo lake ikiwa ni  mwaka huu uishe akiwa amesema ukweli kwa watanzania ili wafahamu kuwa wahusika wa tukio hilo walikuwa na nia ya kumchafua.

sauti ya mbunge gekul

Gekul amesema tuhuma za kuwa alimuingizia chupa sehemu ya haja kubwa kijana huyo si ya kweli na kwamba Daktari aliyempokea na kumpima amebaini hakufanyiwa chochote katika mwili wake.

Amesema tuhuma hizo zilikuja baada ya kijana Hashim ambae alikuwa kama mfanyakazi katika hotel ya palei anayoimiliki mbunge huyo alidaiwa kuwa na kazi maalum ya kumdhuru mbunge huyo na alificha majina yake,namba za simu, vitambulisho na passport size na kudanganya kuwa anaitwa joinathan.

Amesema lengo la kijana huyo ilikuwa ni kumchafua kiongozi huyo ili kushuka kibiashara na kisiasa ambapo amewataka wananchi kuwa na umoja, kuepuka kueneza uvumi, na kushirikiana katika kujenga taifa imara lenye mshikamano.

Aidha, Akiwa kanisani leo, Gekul ameungana na waumini wa Kanisa lake kutoa shukrani kwa Mungu kwa mapito aliyoyapitia ambapo kabla ya shukrani hizo kulitanguliwa harambee ya kanisa na jumla ya shilingi milioni 116 zimepatikana na kati ya hizo zaidi ya shilingi milioni 90 zimekabidhwa kwenye uongozi wa kanisa hilo. Nao baadhi ya viongosi wa dini waliohudhuria ibada hiyo wametumia fursa hiyo kuwaombea viongozi wa Serikali waweze kutimiza majukumu yao kwa uadilifu na kwa kuzingatia maadili wakimtia moyo Mbunge huyo kuendelea kumuamini Mungu siku zote.