FM Manyara

DC Kaganda azindua Mati Foundation

23 November 2024, 8:13 pm

Taasisi isiyokuwa  ya kiserikali ya Mati Foundation yenye lengo la kusaidia wenye uhitaji na  makundi maalumu ikiwemo wenye ulemavu iliyoko chini ya kampuni ya Mati Super Brands Limited imezinduliwa rasmi leo na Mkuu wa Wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda.

Na Mzidalfa Zaid

Akizungumza mara baada ya kuzindua Taasisi ya Mati Foundation, Mkuu wa Wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda  amempongeza Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati Super Brands Ltd David Mulokozi kwa kuisaidia jamii inayomzunguka katika Wilaya ya Babati na Tanzania kwa ujumla kwa kutoa sehemu ya faida anayoipata kusaidia jamii.

sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Mati Foundation ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mati Super Brands Limited David Mulokozi amesema kuwa ndoto yake ni kunyanyua jamii inayomzunguka kwa kurudisha sehemu ya faida anayoipata kwa jamii jambo ambalo limekuwa ni utamaduni wao na ibada pia.

Amesema kampuni hiyo imekuwa ikiunga mkono juhudi za Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan katika kuwahudumia wananchi kupitia misaada mbali mbali wanayoitoa kwa jamii ya Watanzania.

sauti ya Mwenyekiti wa Taasisi ya Mati Foundation ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mati Super Brands Limited David Mulokozi

Nae Mwenyekiti Msaidizi wa Mati Foundation Gwandumi Mpoma amesema kuwa wamekua wakitoa misaada sehemu mbali mbali ikiwemo kwenye maaafa ya Mafuriko hanang,kusaidia fimbo nyeupe kwa wenye ulemavu wa macho pamoja na kutoa misaada kwa yatima,wajane na wazee.

Amesema wametumia kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 1.5 kusaidia jamii inayowazunguka kama mchango wao kwa jamii tangu kiwanda cha Mati Super Brands Limited  kilipoanzishwa mwaka 2017.

sauti ya Mwenyekiti Msaidizi wa Mati Foundation Gwandumi Mpoma

Amesema kampuni hiyo imekuwa ikiunga mkono juhudi za Rais  wa jamhuri ya muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan katika kuwahudumia wananchi kupitia misaada mbali mbali wanayoitoa kwa jamii ya Watanzania.