FM Manyara

Upatikanaji maji vijijini mkoani Manyara wafikia asilimia 71

20 November 2024, 4:39 pm

Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Ruwasa mkoa wa Manyara imesema upatikanaji wa maji katika mkoa wa Manyara kwa vijijini ni asilimia 71 hadi kufikia septemba 30, 2024

Na Mzidalfa Zaid

Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Ruwasa mkoa wa Manyara imesema upatikanaji wa maji katika mkoa wa Manyara kwa vijijini ni asilimia 71 hadi kufikia septemba 30, 2024 ambapo wilaya ya Babati ni asilimia  80.9 Kiteto asilimia 64,Simanjiro asilimia 66.7 Hanan’g ni  asimilia  71.2 na Mbulu  ni asilimia 69.7 sawa na ongezeko la asilimia 14.7 kutoka june 2019  Ruwasa ilipoanza.

Akitoa taarifa hiyo katika  kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Manyara meneja wa Ruwasa mkoa wa Manyara  amesema wakazi wanaohudumiwa na mamlaka hiyo ni millioni 1.5 na wenye maji kati ya hao ni millioni1.06 na ambao hawana maji ya uhakika ni 478,000.9 .

sauti meneja wa Ruwasa mkoa wa Manyara

Amesema katika miradi inayoendelea yenye asilimia 5 hadi 50  ni nane  na asilimia 51 hadi 75 ni mitatu,asilimia 76 hadi 90 ni mitano,asilimia 91 hadi asilimia 100 ni 6 ambapo mkoa una miradi mitano ya kimkakati ikiwemo skimu 303  zinazosimamiwa na vyombo maji ngazi ya jamii.

Aidha amewataka wananchi mkoani Manyara kuendelea kutunza vyanzo vya maji kwa kutofanya shughuli za kiuchumia karibu na vyanzo hivyo ikiwemo kukata miti, kulima au kuchunga mifugo karibu na vyanzo hivyo.