Habari za Jumla
20 January 2023, 7:33 pm
Akutwa mtupu Kanisani Njombe
Mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 40 anayetajwa kuwa ni Mkazi wa Mkoa wa Morogoro amekutwa akiwa mtupu kwenye Madhabahu ndani ya Kanisa la Anglikana lililopo Mtaa wa Matema Halmashauri ya Mji wa Makambako Mkoani Njombe huku…
20 January 2023, 7:23 pm
Miti 5,000 ya Asili yapandwa Kijiji cha Ihela
Wananchi wilayani Makete mkoani Njombe wametakiwa kutunza mazingira ikiwemo vyanzo vya maji ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza ikiwemo kuongezeka kwa joto duniani,ukame pamoja na kubadilika kwa msimu wa mvua. Wito huo umetolewa January 20,2023 na Agustino Ngailo ambaye alikuwa mgeni…
20 January 2023, 7:00 pm
Wananchi 50 Tandala wakabidhiwa Hati Miliki za Ardhi
Ofisi ya Ardhi mkoa wa Njombe imeendesha zoezi la kukabidhi hati zipatazo Hamsini kwa wananchi wa kijiji cha Tandala wilayani Makete pamoja na kusikiliza changamoto za wananchi juu ya zoezi hilo leo Disemba 20 mwaka huu. Emmanuel Mkiwa kutoka ofisi…
20 January 2023, 3:57 am
Madereva Bajaji Walia na Bima
KATAVI Baadhi ya madereva bajaji mkoani Katavi wameeleza namna ambavyo bima za vyombo vya moto haziwasaidii pindi yanapotokea majanga ya barabarani. Wameyaeleza hayo wakati wakipewa elimu juu ya umuhimu wa bima za vyombo vyao vya moto ambapo wamesema aina hiyo…
19 January 2023, 8:03 am
AFUNGWA MIAKA 30 WILAYANI LUDEWA KWA KOSA LA UBAKAJI
Mahakama Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe Januari 17, 2023 imemhukumu kifungo cha Miaka 30 jela Daudi David Mligo, mwenye umri wa miaka 26, mkazi wa Ludewa Mjini baada ya kukutwa na kosa la ubakaji. Mnamo Julai 16, 2022 majira ya saa tisa na dakika…
19 January 2023, 7:53 am
Wajanja wa kurubuni Mbolea kushughulikiwa Njombe
Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka akishirikiana na Jeshi la Polisi mkoani hapa, wamefika katika nyumba ambayo mfanyabiashara wa mbolea amekuwa akitumia kuchakachua bidhaa hiyo. Mtaka amesema katika nyumba hiyo isiyo na umeme, wamebaini mifuko ya makampuni mbalimbali ya mbolea, majenereta…
18 January 2023, 11:07 am
Ujenzi Kituo cha Afya Lupalilo, DC ahimiza Usimamizi
Ujenzi wa Kituo cha Afya Lupalilo awamu ya pili umefikia hatua nzuri baada ya kuwa katika hatua za mwisho wa ujenzi. Kituo hicho ujenzi wake ulianza kwa wananchi kujenga Jengo la wagonjwa wa nje na Serikali ikaunga mkono kwa…
18 January 2023, 10:39 am
Elimu itolewe utunzaji wa Mazingira Makambako-Njombe
Halmashauri ya mji wa Makambako imetakiwa kutoa elimu kuhusiana na usafi wa mazingira ili kuhakikisha maeneo yote yanafanyiwa usafi lengo likiwa ni kukabiliana na magonjwa ambukizi. Wakizungumza na Kituo hiki baadhi ya wananchi wa mtaa wa rajabu mahakamani uliopo…
18 January 2023, 10:04 am
Waziri amfukuza aliyetupa Parachichi Njombe
WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe ameagiza kukamatwa kwa mmiliki wa Kampuni ya Candia Fresh pamoja na kuifunga kampuni hiyo, kwa kile alichoeleza kuwa inanunua parachichi ambazo hazijakomaa. Bashe amesema kuwa kampuni hiyo imekuwa ikinunua parachichi hizo changa na kisha…
17 January 2023, 6:04 pm
Magari ya Shule Kubeba Wanafunzi Kuliko Uwezo.
MPANDA Kutokana na kuendelea kukithiri kwa changamoto ya magari ya shule kubeba wanafunzi idadi kubwa kuliko uwezo, wananchi mkoani Katavi wamewataka wamiliki wa shule kuzingatia sheria zinavowataka. Wakizungumza na mpanda radio fm wananchi wamesema kuwa wameshuhudia baadhi ya magari hayo…