Habari za Jumla
16 January 2023, 7:46 am
Wananchi waiomba Serikali kujenga Barabara Kigulu
Wananchi wa Kijiji cha Kigulu wameiomba Serikali kukamilisha ujenzi wa Barabara ya Kijiji hicho ili kurahisisha shughuli za usafiri na kuongeza mzunguko wa Uchumi kwa wananchi. Wakizungumza mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda wananchi hao…
11 January 2023, 7:47 pm
Elimu ya Utunzaji wa Mazingira kuanza kutolewa Liganga na Mchuchuma Ludewa
Kufuatia kuanza kwa miradi midogo ya uchimbaji madini ya makaa ya mawe wilayani Ludewa mkoani Njombe huku miradi mikubwa ya Liganga na Mchuchuma ikitarajiwa kuanza hivi karibuni shirika lisilo la kiserikali Umbrella of Women and Disabled organization (UWODO) imewasili…
11 January 2023, 7:43 pm
Wananchi elfu 15 Waanza kunufaika na mradi wa Maji Matamba-Kinyika
Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Iringa (IRUWASA) imetekeleza mradi wa Zaidi ya Bilioni moja katika Tarafa ya Matamba na kuukabidhi kwa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Makete Ruwasa mradi huo unatambulika kwa jina la Matamba-Kinyika Makabidhiano…
11 January 2023, 7:39 pm
Wanaume wakatazwa kusimama na Wanafunzi wa Kike Njombe
Serikali wilayani Ludewa mkoani Njombe, imepiga marufuku wanaume kusimama na wanafunzi wa kike kwa zaidi dakika 15 katika mazingira yenye mashaka, baada ya kufanya utafiti mwepesi na kubaini kwamba kuna kundi kubwa la watoto wa kike wanaokatisha masomo kwa…
11 January 2023, 7:37 pm
Wazazi wakamatwe wafanye usafi Shuleni-RC Njombe
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Antony Mtaka amemuagiza mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa kuwakamata na kuwafanyisha usafi kwenye mashuleni pamoja na vituo vya afya wazazi wote ambao watoto wao hawajaripoti shuleni kuanza muhula mpya wa masomo badala ya…
9 January 2023, 6:02 pm
Msikae Ofisini Fuatilieni Ufundishaji na Ujifunzaji Mashuleni: Dkt. Dugange
Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo J. Dugange amewataka viongozi wa Elimu ngazi ya Shule, Kata, Halmashauri na Mikoa kutokaa ofisini bali wafuatilie ufundishaji na ujifunzaji shuleni kwa kushauriana na walimu na kuhakikisha wanafunzi wanapata umahiri…
9 January 2023, 5:27 pm
Msako kuanza kwa Wazazi/Walezi ambao hawajapeleka Wanafunzi Shule
Wanafunzi Kidato cha kwanza na darasa la kwanza wameanza kuripoti shuleni katika shule mbalimbali Wilayani Makete huku Mkuu wa Wilaya akiagiza kukamatwa kwa Mzazi yeyote ambaye hataki kupeleka mwanafunzi shuleni. Leo tarehe 9 Januari, 2023 Akiwa katika ukaguzi wa…
7 January 2023, 8:32 pm
Mwanafunzi hata kama hana Sare aanze Masomo-dc Mhe. Sweda
Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda amekagua vyumba vya madarasa kwa shule za Sekondari ambavyo wanafunzi wataripoti na kuanza masomo Januari 9, 2023. Mhe. Sweda amesema Serikali imehakikisha wanafunzi wanapata Mazingira rafiki ya kujifunzia na hivyo mpaka…
7 January 2023, 7:28 pm
Miundombinu imekamilika kupokea Wanafunzi Januari 9, 2023- Mhe. Mpete
Wakati shule zote nchini Tanzania zikitarajiwa kufunguliwa siku ya Jumatatu ya Januari 9 ,2022 wazazi na walezi mkoani Njombe wametakiwa kuwaandalia watoto mahitaji yote muhimu ili wanafunzi wote waripoti shule na kuanza masomo kwa pamoja. Akizungumza na wanahabari Mwenyekiti…
7 January 2023, 7:19 pm
Serikali kutafuta namna ya Kumkopesha Mwananchi Simu Janja
Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhe.Nape Nnauye ( Mb ) amesema serikali iko mbioni kutafuta namna ya kumuwezesha mtanzania wa kawaida kumudu gharama ya kununua simu janja. Amebainisha hayo wakati akizindua mnara wa simu katika Kijiji cha Kinenulo…