Adhana FM

Masheha simanieni sheria na utawala bora- RC Kaskazini Unguja

8 June 2024, 5:19 pm

Na Abdul Sakaza, Mkoa Kaskazini Unguja

Masheha katika mkoa wa kaskazini Unguja wametakiwa kufanya kazi kwa kufuata misingi, sheria na uadilifu ili kukuza utawala bora katika jamii.

Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa Kaskazini Unguja Hadidi Rashid Hadidi wakati alipokua akizungumza na masheha wa mkoa huo, ofisini kwake Mkokotoni.

RC Hadidi ameeleza kua, kunabaadhi ya masheha hawafuati sheria katika uongozi wao jambo ambalo linaweza kurudisha nyuma shuhuli mbali mbali za kijamii na serikali kwa ujumla.

Amewaambia masheha kufuata miongozo ya viongozi wao na kuepuka mambo yanayorejesha nyuma jamii kama vile kutumika kisiasa, kutoa matamko yasio faa kwa wananchi na kusingia kua maagizo kutoka kutoka kwa viongozi wakuu wa nchi.

Kwaupande wao masheha wa mkoa huo wamesema watahakikisha wanafuata sheria na uadilifu katika kazi zao ili kuwahudumia wananchi katika misingi ya sheria na utawala bora.