Rais Mwinyi awaongoza Waislamu kwenye Hawli ya kutimiza miaka 100 tokea kufariki mwanachuoni Sheikh Sayyid Omar Qullatein
27 September 2023, 9:15 pm
Na Ali Khamis – Zanzibar
Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi ametoa ujumbe wa kushikamana na kupendana alipojumuika na waumini wa kiislam katika hafla ya hawli ya kutimiza miaka 100 tokea kufariki Sheikh Sayd Oamr Qullatein, shughuli iliyoandaliwa na familiya yake katika msikiti wa ijumaa Mlindi Zanzibar.
Katika hawli hiyo iliyosimamiwa na ofisi ya Muft mkuu wa Zanziabr, Rais mwinyi aliwasissitiza waumini wa kiislamu kuwatukuza wanawazuoni ili kuendeleza tabia zao njema kwani kazi za elimu walizozifanya muda wote zimeleta mwangaza na uongofu katika jamii.
Alhabib Muhammad Bin Syyid Hussein Alhabshi kutoka Yemen amesema kuwa hakuna hadhara kubwa kama waislamu kushikamana na kukusanyika pamoja kwa kumtaja Allah na Mtume wake Muhammad S.A.W na kuwatakia kheri wanazuoni ambapo amefurahi kuwa mkusanyiko huo mkubwa kwa ajili ya mwanachuo huyo ujumesadifu katika mwezi mwema wa kuzaliwa kwa Mtume S.A.W.
Sheikh Abdinur Abdillah Muhamed kutoka Kenya amlizungumzia kuhusu ukweli na kusema kuwa makamo ya ukweli ni makamo makubwa ambapo amefafanua jambo hilo kwa kusema kuwa baada ya daraja ya ukweli ni makamo ya Mtumbe S.A.W na kuwataka waumini kushikamana na ukweli kwakua sheikh Qulllateni alikua ni mtu mkweli.
Naye mwanafamilia, Sayyid Mudhihiridin bin Ally Qullatein alitoa tarjama ya historia ya uzao ya sheikh Sayyid Omar Bin Muhammad Bin Mudh-Hir Qulaltein Al-Nadhiyr Baalawiy mwanachuoni huo mtajika ambapo amesema kuwa Sheikh Uwesu Alqadiry alimpa ijaza ya ukhalifa wa twariqa Sheikh pamoja na masheikh wengine watano kwa hapa Unguja ambao ni Sheikh Said Othamn, Sheikh Mjanakheri, Sheikh Haji Mshenga, Sheikh Hamdou na Sheikh Shauri.
Hafla hiyo iliyofungwa kwa dua na Muft Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi, ilihudhuriwa na Makamu wa Kwanza wa Rais – Otman Masoud Othman, Waziri wa Nchi ofisi ya Rais katiba, sharia, Utumishi wa uma na utawala bora – Haroun Ali Suleiman, Mkuu wa mkoa wa Mjini magharib Idrisa Kitwana Mustafa, masheikh kutoka nchi mbali mbali pamoja na waumini kutoka hapa Zanzibar.