Vwawa FM Radio
Vwawa FM Radio
November 20, 2025, 3:02 pm

Asajile amekuwa akiwasoma Ng’ombe wake tabia hii humsaidia kupata maziwa kwa wingi zaidi
Na Anyisile Fredy
MKAZI na mfugaji wa ng’ombe wa maziwa mjini Vwawa Mbozi Mkoani Songwe, Mikaya Asajile amesema amewagundua ng’ombe wake kwamba wanapenda muziki wakati wa kukamuliwa.
Amesema hayo alipozungumza na Vwawa Fm iliyoshuhudia muziki kwenye zizi wakati Asajile akiwakamua ng’ombe hao.
Mfugaji huyo ambaye ni kijana asiyependa uzururaji bali kazi za kilimo na ufugaji amesema awali alikuwa akiwapa pumba ng’ombe wake wakati wa kuwakamua, lakini sasa anatumia muziki.
Asajile ambaye ana mke na watoto na mcheshi wa tabia amesema amekuwa akiwasoma ng’ombe wake tabia kwani wanatofautinana. Amesema aliloligundua kwa ng’ombe wake ni kupenda burudani.
Ametaja aina ya muziki wanaopenda n’gombe wake.