Vwawa FM Radio

EFAD yagusa maisha ya watoto Songwe

September 26, 2025, 9:07 am

Mkurugenzi wa EFAD Elisha Shombe(kushoto) akimkabidhi chakula Afisa maendeleo Tumpale Mndekesye(kulia). Picha Na Devi Mgale

Kupunguza utoro shuleni na kuongeza utulivu wa watoto shuleni

Na Devi Mgale

Shirika lisilokuwa la kiserikali la Elisha Youth Support Foundation (EFAD) lililopo wilaya ya Mbozi mkoa wa Songwe limetoa kilo 420 za Mahindi kwa watoto wanaoishi mazingira magumu katika shule ya msingi Mtumbo wilayani hapa

Mkurugenzi wa Shirika hilo Elisha Shombe, amesema wamejikita kusaidia vijana na watoto wanaokabiliwa na changamoto za kijamii na kiuchumi. Amesema lengo kuu la kutoa msaada huo ni  kupunguza utoro shuleni.

Sauti ya Elisha Shombe

Naye Katibu wa EFAD Omary Kaita, amesema ina jukumu la kuikumbusha jamii umuhimu wa kushirikiana katika kuonyesha utu wa kiafrika na kuthamini vijana ambao ndio taifa la kesho.

Sauti ya Omary Kaita

Kwa upande wake, Mjumbe wa EFAD, Gille Jalileni, amewataka wazazi na walezi kuona umuhimu wa kutoa chakula kwa watoto. Ameongeza kuwa licha ya wilaya ya Mbozi kujulikana kwa uzalishaji mkubwa wa mahindi, bado muitikio wa wazazi kuhusu elimu ni mdogo.

Sauti ya Gille Jalileni