Uvinza FM

Walaji wa wanyama wa mwituni hatarini kupata marburg

5 March 2025, 12:00 am

Afisa Afya na Mratibu wa Elimu ya afya kwa umma wa wilaya ya uvinza Dk. Mulla Mnyanyi akitoa elimu ya ugonjwa wa marburg katika studio ya uvinza fm redio. (Picha na Ezra Meshack)

Ameseama jamii inapaswa kuchukua tahadhari kwa kuepuka kugusa au kula nyama ya popo, au nyama ya mnyama wa mwituni akiwemo nyani.

Na Theresia Damasi

Wananchi wa Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma na maeneo ya jirani wameshauriwa kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa marburg ambao kwa sasa ni ugojwa hatari unaoua kwa haraka kama ilivyoripotiwa katika baadhi ya nchi za Afrika na Afrika Mashariki.

Akizungumza na Radio Uvinza FM Afisa Afya na Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma wa Wilaya ya Uvinza Dkt. Mulla Mnyanyi ameeleza namna ugonjwa unavyoambukizwa .

Sauti ya Afisa Afya 1

Mnyanyi  ameendelea kwa kusema kuwa ugonjwa wa marburg ni familia moja na virusi vya ebola ambapo ameeleza dalili zake.

Sauti ya Afisa Afya 2

Aidha afisa Mulla Mnyanyi amesema umhimu wa kuchukua hatua stahiki za kwenda hospitali pale mtu anapoona dalili za ugonjwa wa marburg.

sauti ya afisa 3

Hata hivyo Dkt. Mulla amesema jamii inapaswa kuchukua tahadhari kwa kuepuka kugusa au kula nyama ya popo, au nyama ya mnyama wa mwituni akiwemo nyani, kuosha mikono kwa maji safi mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni, kutokushika mgonjwa mwenye ugonywa wa marburg.