

28 February 2025, 4:20 pm
Wafanyakazi wa Uvinza FM wamepatiwa elimu juu ya ugonjwa wa marburg na namna ya kujilinda na ugonjwa huo.
Na Linda Dismas
Msimamizi wa vipindi wa Uvinza fm Bw. Abdunuru Shafii ameeleza namna ambavyo ugonjwa wa Marburg unaenezwa pamoja na kuwataka wafanyakazi wake kujilinda dhidi ya ugonjwa huwo.
Ameyasema hayo wakati akitoa elimu kwa wafanyakazi hao na kusema kuwa ugonjwa wa marburg unaambukizwa kwa njia nyingi na moja ya njia hizo ni pamoja nakuchangia vitu vyenye ncha kali na mtu mwenye maambukizi ya ugonjwa huwo.
Ameendelea kwa kusema kuwa kuna baadhi ya wanyama kama vile popo,tumbili,nyani na sokwe wanaishi na ugonjwa huwo hali ambayo inapelekea binadamu kupata ugonjwa huwo pale ambapo atakula au kugusa mzoga wa wanyama wenye virusi vya ugonjwa huwo.
Aidha Bw. Shafii amesema kuwa ugonjwa wa marburg huaanza kuonekana kati ya siku 2 hadi 21 baada ya mtu kupata maambukizi ya ugonjwa huwo, na moja ya dalili hizo ni pamoja na kupata maumivu ya kichwa, kutokwa na damu sehemu za wazi mfano puani, machoni, puani na kadhalika.
Sambamba na hayo amesema kuwa kuna njia nyingi za kujikinga na ugonjwa huwo na moja ya njia hizo ni mtu kuepuka kugusana na mtu mwingine kwa kupeana mikono, kukumbatiana wakati mwingine hata kubusiana.
Bw.Shafii amemalizia kwa kuwataka wafanyakazi wake kuwa mstari wa mbele kwa kuhakikisha wanaendelea kutoa elimu ya ugonjwa wa marburg kwa wananchi wengine ili kutokomeza ugonjwa huwo wa marbug.
Ikumbukwe kuwa kinga ni bora kuliko tiba hivyo basi endapo ukipata dalili za ugonjwa huu piga simu 199 bure kwa msaada zaidi.