Uvinza FM

Wanafunzi wapata mafunzo kwa vitendo

24 February 2025, 11:11 pm

Picha ya wanafunzi pamoja na walimu wa shule ya msingi Nyambutwe wakiwa katika studio ya Uvinza fm (Picha na Ezra Meshack)

Wanafunzi wamepata mafunzo ya namna ya urushaji wa matangazo redioni, ikiwa wapo katika kujifunza mada ya Antena.

Na Theresia Damas

Wanafunzi katika shule ya msingi Nyambutwe wilayani uvinza wamepata mafunzo ya namna ya urushaji wa matangazo redioni, ikiwa wapo katika kujifunza mada ya Antena katika somo la sayansi.

Wakizungumza mara baada ya mafunzo wanafunzi hao wamesema wamepata maarifa maakubwa baada ya kujifunza kwa vitendo huku wakiwaomba walimu kutenga mda wa kutembelea maeneo ili kujifunza kwa vitendo Zaidi.

Sauti ya wanafunzi.

Kwa upande wake Jane Ndalichako mwalimu mkuu wa shule hiyo  amesema amefurahishwa  na kitendo cha wanafunzi wake kupata mafuzo  kwa vitendo kwani yatawasaidia  Zaidi katika kumbukumbu zao na kujiongezea maarifa.

Sauti ya Mwalimu Ndalichako.

Ameendelea na kusema kuwa wakazi wa wilaya ya uvinza na viunga vyake watumie fursa ya kutangaza biashara zao na kueleza changamoto zinazowasibu  kupitia redio jamii uvinza fm.

Sauti ya Mwalimu Ndalichako.

Naye  mwalimu Salehi Hamisi Mteka ameishukuru redio uvinza fm kwa kuweka vipindi vya watoto ambavyo vinatoa elimu mbalimbali ikiwemo masuala ya ukatili huku akiwaomba wazazi kuwaruhusu watoto wao kuhudhuria vipindi pale wanapohitajika kujifunza.

Sauti ya Mwalimu Salehi Mteka.