Uvinza FM

Ukosefu wa mfumo wa utiririshaji maji kilio kwa wananchi

22 February 2025, 6:59 pm

Afisa Mtendaji kata ya Uvinza Bw. Edward Amos akifafanua juu ya ukosefu wa mfumo wa utiririshaji maji (Picha na Linda Dismas)

Wananchi mkoa wa Kigoma walia na serikali juu ya ukosefu wa mfumo wa utiririshaji wa maji wadai kunawapelekea kupatwa na magonjwa ya mlipuko.

Na Linda Dismas

Wananchi wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma wameeleza changamoto wanazokumbana nazo kutokana na kutokuwa na mfumo wa utiririshaji maji.

Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Uvinza fm na kueleza kuwa kutokuwa na mfumo wa utiririshaji maji kunawapelekea kupatwa na magonjwa ya mlipuko.

Sauti za Wananchi.

Aidha wameuwomba uwongozi wa mtaa huo kuhakikisha wanawajengea miundombinu thabiti kwa ajili ya kupitisha maji hayo.

Sauti za Wananchi.

Naye Afisa mtendaji wa kata ya Uvinza Bw.Edward Amos amedhibitisha kuwa kuna baadhi ya barabara hazina mitaro huku changamoto ikiwa ni bajeti ya TARURA.

Sauti ya Mtendaji.

Bw.Amos amesema moja ya kitongoji ambacho kinakumbana na changamoto ya ukosefu wa mitaro ni pamoja na kitongoji cha Lugongoni.

Sauti ya Mtendaji.

Aidha ameeleza kuwa huwa wanashirikiana na wananchi ili kutatua changamoto ya kukosekana kwa mfumo wa utiririshaji maji.

Sauti ya Mtendaji.