Mazingira machafu mighahawani yanavyohatarisha maisha ya watu
25 January 2025, 5:04 pm
Mama n’tilie wakiendelea na shughuli zao za kupika chakula. Picha kutoka maktaba
Walaji wa vyakula vya mighahawani walia na changamoto wanazozipata kutokana na vyakula hivyo.
Na Kelvin Mambaga
Wananchi wa wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma wameeleza namna ambavyo mazingira ya mighahawani si rafiki kwa afya zao.
Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Uvinza FM na kueleza kuwa kuna baadhi ya wahudumu wa mighahawa hawazingazii kanuni za usafi wa vyakula hali inayowapelekea wao kama walaji kupata changamoto za kiafya.
Kwa upande wake Dkt. David Samson kutoka Hospitali ya Wilaya Uvinza amebainisha kuwa vyakula ambavyo si salama kwa afya ya mlaji ni vyakula visivyozingatia usafi katika uandaaji.
Dkt. David ameongeza kwa kusema kuwa ulaji wa vyakula visivyozingatia usafi unasababisha magonjwa hatari kama vile kipindupindu, kuhara na magonjwa mengi ya tumbo.