Wilaya ya Kasulu yatoa mkopo wa zaidi ya milioni 493
16 January 2025, 5:24 pm
Wanufaika wa mikopo hiyo wametakiwa kuzitumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa kwa ajili ya kuleta maendeleo ya familia zao.
Na Emmanuel Kamangu
Halmashauri ya wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma imekabidhi hundi ya mkopo wa zaidi ya shilingi milioni 493 kwa vikundi 21 kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.
Katika Hafla hiyo ya kukabidhi mikopo ya asilimia 10 ambayo imetolewa katika kipindi cha robo ya pili kuanzia mwezi oktoba hadi disemba 2024/2025 inalenga kunufaisha vikundi 21 vya halmashauri hiyo
Akizungumza katika hafla hiyo Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu Bw Eliya Kagoma amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kuzitumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa kwa ajili ya kuleta maendeleo ya familia zao.
Sauti ya Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu Bw Eliya Kagoma
Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu Dkt Semistatus Mashimba amesema mikopo hiyo inalenga kuinua uchumi wa jamii katika kufanya shughuli za maendeleo.
Sauti ya Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu Dkt Semistatus Mashimba
Mkuu wa division ya maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Kasulu Victoria Moses amesema halmashauri inawajibu wa kuhakikisha mikopo hiyo inatolewa kwa wananchi waliokidhi vigezo na kuwataka kurejesha mikopo hiyo kwa wakati.
Sauti ya Mkuu wa division ya maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Kasulu Victoria Moses
Nao baadhi ya wanufaika wa mikopo hiyo wameishukuru serikali na kueleza namna itakavyowasaidia kuendesha maisha yao.
Sauti za baadhi ya wanufaika wa mikopo hiyo