Jamii yaaswa kula mboga za majani kuepuka magonjwa
15 January 2025, 10:11 pm
Kwa sababu mboga za majani zina madini mbalimbali yanayosaidia katika kuimarisha afya kwa ujumla.
Na Emmanuel Kamangu
Jamii katika halmashauri ya mji wa Kasulu mkoani Kigoma imeshauriwa kujenga tabia ya kula mbogamboja za majani kwa ajili ya kuimalisha mfumo wa kinga za mwili.
Amesema hayo afisa Lishe halmashauri ya mji wa kasulu Bw, Mwita chacha Range wakati akizungumza na uvinza fm ambapo amebainisha kuwa jamii ili kuweka vizuri utendaji wa mwili kuna kila sababu za kuweka kipaumbele cha ulaji wa mbogamboga za majani.
Aidha Bw, Range amesema kuwa wa mama wajawazito wakiwemo makundi rika wanapaswa kula mboga za majani kwa wingi ili kuimalisha miili yao na kuikinga dhidi ya magonjwa.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa halamshauri ya mji wa kasulu wamesema licha ya wataalamu wa afya kuendelea kutoa elimu juu ya wao kuelewa umuhimu wa ulaji wa mboga za majani ila bado waliowengi elimu haijawafikia jambo linalopelekea kuelewa kuwa kula mboga za majaji ni umasikini.
Hata hivyo wameiomba serikali kuweka hamasa kwa kila kaya walau kuwa na bustani ya mboga za majani kwa ajili ya kula ili kuimalisha afya zao.