Uvinza FM
Uvinza FM
18 March 2026, 3:15 pm

Wanyamulenge imempongeza Rais Evariste Ndayishimiye kwa juhudi zake za kusimamia amani nchini DRC,kusaidia na kuwajali watu wa Kongo
Na. Bukuru Daniel
Jamii ya Wanyamulenge kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokarsia ya Kongo wamempongeza Rais Evarsite Ndayishimiye katika jukumu la serikali yake la kulinda amani nchini DRC na kupambana na waasi wa
Wakizungumza na vyombo vya habari mjini Bujumbura magaharibi mwa Burundi,jamii hiyo ya Wanyamulenge imempongeza Rais Evariste Ndayishimiye kwa juhudi zake za kusimamia amani nchini DRC,kusaidia na kuwajali watu wa Kongo, ikiwa ni pamoja na watu kutoka jamii hiyo ambao walikimbilia Burundi.
Charles Nteze kiongozi wa shirika la Wanyamulenge Global Advocacy kwasasa akiwa anaishi Marekani, amesema Burundi imepiga hatua kubwa katika kupambana na waasi wa M23 wanaodaiwa kufadhiliwa na serikali ya Rwanda licha ya serikali ya Kigali kukanusha mara kadhaa.
Hata hivyo mashirika mengine kutoka jamii ya Wanyamulenge wanaoishi nje ya nchi hivi karibuni yalitoa taarifa za kulaani mauaji ya ndugu zao huko Minembwe, na kusema kuwa wanajeshi wa Burundi ni miongoni mwa waliohusika.