Uvinza FM

Wananchi andamaneni kupiga kura sio kuvunja amani Kigoma

22 October 2025, 8:47 pm

Kamishna msaidizi mwandamizi Emmanuel Makungu akizungumza na wananchi katika studio za Uvinza fm.

Wananchi acheni kudanganyana kuandamana bila sababu za msingi bali mnatakiwa muandamane kwenda kupiga kura na kuwachagua viongozi sahihi.

Na Theresia Damasi

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa kigoma Kamishna msaidizi mwandamizi Emmanuel Filemon Makungu amewataka wananchi wa mkoa wa Kigoma kuwa watulivu kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 octoba mwaka huu.

Amesema uchaguzi ni kitendo cha wananchi kutimiza wajibu wao wa kupiga kura bila kuzua taharuki ambazo zitavunja hali ya usalama katika siku ya hiyo.

Kamishina Makungu ameyasema haya wakati akizungumza na Radio Uvinza fm katika kipindi cha Kumekucha ambapo amesema wananchi waache kudanganyana kuandamana bila sababu za msingi bali wanatakiwa waandamane kwenda kupiga kura na kuwachagua viongozi sahihi.

Sauti ya kamanda Kamishna msaidizi mwandamizi Emmanuel Filemon Makungu 1

Aidha Kamishna huyo amesema pale mwananchi anapoona viashiria vya uvunjifu wa amani anapaswa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi ili hali hiyo iweze kudhibitiwa haraka iwezekanavyo.

Sauti ya Kamanda msaidizi mwandamizi Emmanuel Filemon Makungu 2

Pamoja na hayo Jeshi la polisi mkoa wa Kigoma limesema limejiandaa vyema kulinda usalama wa raia na mali zao katika kipindi cha uchaguzi hivyo wananchi wajitokeze kwa wingi kupiga kura oktoba 29 mwaka huu.