Uvinza FM
Uvinza FM
20 October 2025, 6:54 pm

wananchi mfike kwenye vituo vya kupiga kura ili kutambua mapema kama majina yenu yapo kwenye orodha
Na Emmanuel kamangu
Wananchi wilayani kasulu wamearifiwa kuhakikisha wanafahamu kwa wakati vituo watakavyopigia kura kabla ya siku yenyewe ya octoba 29 ambayo ni siku ya kuwachagua madiwani , wabunge na Raisi.
Akizungumza na wandishi wa habari msimamizi wa uchaguzi jimbo la kasulu vijijini Bw, Emmanuel Ladslausi amesema vituo vya uchaguzi vitafunguliwa saa moja asubuhi na kufunga saa kumi jioni ili kutoa fursa kwa wananchi waliowengi kupiga kura.
Aidha Bw, Ladslausi amewataka wananchi kufika katika vituo vyao vya kupiga kura ili kutambua mapema kama majina yao yapo kwenye orodha ya kuwachagua madiwani, Wabunge na Raisi.
Hata hivyo Bw, Ladslaus amesema kwa wananchi ambao wamepoteza vitambulisho vya mpiga kura wataruhusiwa kuchagua endapo watakuwa na Lesen ya udereva au kitambulisho cha Nida.
Jimbo la uchaguzi la kasulu vijijini linajumula ya vyama sita vya siasa ambavyo vinashiriki uchaguzi huu wa octoba 29,huku kila chama kikiendelea kunadi sera zake ili kupata ridhha ya kuwaongoza wananchi.