Uvinza FM
Uvinza FM
2 October 2025, 3:55 pm

Hili ni zoezi la utoaji wa fomu za mfano za kuweka tiki kwa mgombea atakaye chaguliwa, ili iwe rahisi kutumika katika mikutano ya ugombea udiwani wakati wa kunadi sera zao.
Na Dunia Stephano
Msimamizi wa uchaguzi ambaye pia ni mtendaji kata ya Uvinza Edward Amosi Nkanga amewataka wananchi kuwa na imani na tume huru ya uchaguzi wakati wa kupiga kura ukifika na waachane na kauli ya kulinda kura kwani ni kiashiria cha uvunjifu wa amani.
Amesema hayo ofisini kwake alipokuwa akifanya mazungumzo na uvinza fm wakati wa utoaji wa form za mfano za kuweka tiki kwa mgombea watakao mchagua ili iwe rahisi kutumika katika mikutano ya ugombea udiwani wa kata hiyo kutumia kuonesha watakavyo piga kura .
Sauti msimamizi wa uchaguzi kata
Aidha mgombea udiwani kupitia tiketi ya chama cha Act wazalendo ameahidi kuwa atawaunganisha wananchi wa Uvinza kuwa kitu kimoja bila kujali itikadi ya vyama, dini wala kabila .
Sauti Himidi kisobwe
Kwa upande wake mgombea udiwani kupitia tiket ya chama cha mapinduzi CCM Nilis Ntabaye amewahakikishia wananchi wa Uvinza maendeleo pindi atakapopewa ridhaa ya kuwa diwani wa kata ya hiyo.

Sauti nilisi noel ntabaye
Ikumbukwe kuwa zoezi hilo ya kukabidhiwa fomu za mfano kwa wagombea zimetolewa na tume huru ya uchaguzi kwa malengo ya wagombea vyama vya siasa kutumia kama sehemu ya kuwaonesha wafuasi wao namna ya kupiga kura .