Uvinza FM

Wananchi watakiwa kuripoti wanaotoa na kupokea rushwa Uvinza

22 August 2025, 6:51 pm

Picha Afisa kutoka TAKUKURU akitoa elimu ya kupambana na rushwa kwa wananchi katika studio za uvinza redio.

Wananchi watoe ushirikiano watakaobaini vitendo vya rushwa vikifanyika kwa wagombea na wananchi kuelekea uchaguzi 29 Octoba 2025.

Na Theresia Damasi

Wananchi wa wilaya ya uvinza mkoa wa kigoma wametakiwa kuripoti taarifa za wale wote wanaojihusisha na utoaji na upokeaji wa rushwa katika ofisi za Takukuru kuelekea uchaguzi mkuu octoba 29, 2025.

Wito huo umetolewa na Afisa Takukuru wilaya ya uvinza Bw. Ibrahim Mtangoo wakati akizungumza na uvinzafm ambapo amesema wananchi watoe ushirikiano watakaobaini vitendo vya rushwa vikifanyika kwa wagombea na wananchi.

Sauti Afisa Mtangoo

Aidha Bw. Mtangoo amesisitiza kuwa endapo wananchi watapokea rushwa watashindwa kupata kiongozi aliye sahihi atakayeleta maendeleo na kufanya kazi kwa weledi.

Sauti Afisa Mtangoo

Hata hivyo Uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu, ambapo wananchi watapata fursa ya kuchagua viongozi wanaowaamini kuwatumikia katika nafasi mbalimbali za uongozi.