Uvinza FM
Uvinza FM
20 August 2025, 11:11 pm

Mgombea katika nafasi ya udiwani kata ya uvinza kupitia chama cha mapinduzi CCM amewaahidi wananchi kuwa mtiifu na kuwaletea maendeleo endapo akifanikiwa kuchaguliwa.
Na Theresia Damasi
Wananchi wa kata ya uvinza wilaya ya uvinza mkoa wa kigoma wametakiwa kujitokeza kupiga kura ifikapo tarehe 29 Oktoba 2025 ikiwa ni sehemu ya kutekeleza wajibu wao kwa kupiga kura kama raia.
Akizungumza na uvinza fm Bw. Nilis Noa Ntabaye ambaye ni mgombea katika nafasi ya udiwani kata ya uvinza kupitia chama cha mapinduzi CCM ambapo amewaahidi wananchi kuwa mtiifu na kuwaletea maendeleo endapo akifanikiwa kuchaguliwa.
Sauti ya mgombea wa chama cha mapinduzi CCM
Bw. Ntabaye amesema amepitia mchakato wa kura za maoni ya kupata ridhaa ya nafasi hiyo, hivyo anaamini wananchi wanamatumaini naye ambapo amewaahidi kuwa hatawaangusha.
Kwa upande wake Afisa mtendaji wa kata ya uvinza na mwakilishi wa Tume huru ya uchaguzi Bw. Edward Amos Nkanga amesema wagombea ambao wamepata ridhaa yakuwawakilisha wananchi katika kata zao wanapaswa kufuata utaratibu waTume huru ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na kufanya kampeni zao kwa Amani.
Sauti ya Mwakilishi wa Tume ya Uchaguzi
Hata hivyo Uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu, ambapo wananchi watapata fursa ya kuchagua viongozi wanaowaamini kuwatumikia katika nafasi mbalimbali za uongozi.