Uvinza FM
Uvinza FM
14 June 2025, 10:24 am

Kanisa linahitaji wanaume wa kutosha na wenye moyo thabiti wa kulitunza kanisa la Mungu.
Na Emmanuel Kamangu
Wanaume wa kanisa katoliki parokia ya mrubona jimbo katoliki la kigoma wametakiwa kuwa kielelezo cha kanisa ikiwemo kusimama imara katika kulifanya kanisa kuwa na umoja.
Amesema hayo paroko wa parokia ya Mrubona Kasulu mjini Padre Gaspa Balkumutwe katika misa takatifu ambayo imeambatana na sherehe za utume wa wanaume wa katolki Uwaka parokiani apo ambapo ameleleza kuwa kanisa linahitaji wanaume wa kutosha na wenye moyo thabiti wa kulitunza kanisa la Mungu .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa wanaume wa katoliki Uwaka Parokia ya Mrubona Bw Camilius Tomas amesema wanapokutana wanaume wakatoliki na kufanya hafla mbali mbali ni moja ya kuendelea kujenga umoja ikiwemo kutiana moyo katika kuendelea kushiriki matendo ya huruma kwa kuwatunza wahitaji wenye shida mbali mbali.
Nao baadhi ya wanaume wakatoliki ambao wameshiriki katika kutaniko hilo wamesema wamepokuwa na sherehe za mara kwa mara za uwaka huwasaidia kukua kiimani pamoja kuwavuta wanaume wengi zaidi kuingia katika utume huo. Hata hivyo wanaume hao wakatoliki wameongeza kuwa wanawajibu wa kuchochea maendeleo ya kanisa .