Uvinza FM

RPC Kigoma akemea migogoro ya wafugaji na wakulima

23 January 2025, 1:08 pm

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kigoma ACP Philemon Makungu picha kutoka maktaba

Mtu yeyote atakaye ingiza mifugo yake kwenye shamba la mkulima hatua kali zitachukuliwa.

Na Linda Dismas

Wakazi katika kijiji cha Nyambutwe wilayani Uvinza mkoa wa Kigoma wameiomba serikali kumaliza migogoro baina ya wakulima na wafugaji.

Hayo yamesemwa na baadhi ya wakazi kijijini hapo wakati wakizungumza na Uvinza Fm na kueleza kuwa serikali inapaswa kugawa maeneo kwa wakulima na wafugaji ili kuepuka changamoto hiyo.

Sauti ya Wananchi.

Naye kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kigoma ACP Philemon Makungu amedhibitisha kuwepo kwa migogoro hiyo baina ya wafugaji na wakulima, na kusema kuwa kitendo cha mfugaji kuvamia eneo la mkulima sio migogoro bali ni uhalifu.

Sauti ya ACP Philemon Makungu.

Aidha Kamanda Makungu ametoa wito kwa wakulima kwa kuwataka kutoa taarifa eneo husika mara baada ya kubaini kuwa wameharibiwa mazao yao na wafugaji.

Sauti ya ACP Philemon Makungu.

Sambamba na hayo amesema kuwa hata hivyo serikali imejipanga kuwaelimisha wafugaji na wakulima na kwamba wamekwisha kugawa baadhi ya maeneo kwaajili ya wafugaji.

Sauti ya ACP Philemon Makungu.