Ukosefu mitaro ya maji yawakero kwa wananchi kata ya Mwanga
4 July 2023, 11:27 am
Wananchi wa kata ya mwanga manispaa ya kigoma uiomba TARURA kurekebisha mitaro ya maji kulingana na adha wanayoipata ya kukatika kwa barabara wakati wa mvua
Na Glory Kusaga
KIGOMA.
Baadhi ya Wananchi wa Mtaa wa Kilimahewa B Kata ya Mwanga Kusini Manispaa ya Kigoma Ujiji wemeomba Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini TARURA kukarabati mitaro ya barabara za mtaa huo kwani baadhi ya barabara zimekatika kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha.
Wananchi hao wa Mtaa Kilimahewa wamesema mitaro ambayo imewekwa kwa baadhi ya barabara za mtaa huo haikuzingatia ubora hali ambayo imepelekea barabara kukatika na kusababisha baadhi ya shughuli kushindwa kufanyika hususani usafirishaji.
Tushafika eneo hilo na kuona miundombinu ya mitaro ilivyo haribiwa na Mvua zikipungua tutafanya ukarabati wa mitaro hiyo
Naye Afisa Mtendaji wa Kata ya Mwanga Kusini, Ramadhan Kalukula amesema changamoto ya barabara za mitaa kukatika wanaifahamu wamekwishapeleka taarifa hizo ofisi ya tarura kwa ajili ya ukarabati.
Akitolea ufafanuzi suala hilo Meneja wa Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini TARURA Wilaya ya Kigoma Mhandisi Paul Mtapima amesema wameshafika eneo hilo na kuona miundombinu ya mitaro ambayo imeharibiwa na Mvua na kuwa Mvua ikipungua watafanya ukarabati wa mitaro hiyo.