Siku ya wanawake duniani jamii yaaswa kujitokeza kuiadhimisha
24 February 2022, 4:36 pm
Na,Rosemary Bundala
Kuelekea siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika tarehe nane mwezi wa tatu kila mwaka jamii imeaswa kujitokeza katika kuadhimisha maadhimisho hayo
Hayo yamezungumzwa na afisa maendeleo ya jamii kutoka wilaya ya uvinza Mkoani Kigoma bi MASTIDIYA NDYETABULA wakati akizungunmza na redio uvinza fm katika kipindi cha Amka na Uvinza fm ambapo ameitaka jamii kubadirika na kufuata utaratibu ili kuleta usawa wa maendeleo endelevu katika jamii
Aidha afisa huyo wa maendeleo amewata kinababa pamoja na vijana kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho hayo kwani siku hii haiwalengi kina mama peke yao
Katika hatua nyingine bi MASTIDYA amewataka wanawake kuitumia siku hii kama siku ya kuacha kufanya matendo maovu , ili waweze kudumisha mahusiano yenye usawa
Maadhimisho Siku ya wanawake duniani ilianza kutokana na jitihada za wanawake 15000 mwaka 1908 walio andamana mjini newyork Marekani , wakidai kupunguziwa muda wa kufanya kazi , kulipwa ujira mdogo na haki ya kupiga kura na ikumbukwe kauli mbiu ya siku hii ya wana wake duniani kwa mwakaa huu 2022 ni Kizazi cha haki na usawa kwa maendeleo endelevu.