Uvinza FM

Wafanyabiashara waishukuru serikali kwa kuondoa vikwazo vya kufanya biashara

19 August 2021, 4:45 pm

Na,Glory Paschal

Wafanyabiashara katika halmashauri ya mji wa Kasulu mkoani Kigoma wameishukuru serikali  kupitia  mamlaka ya mapato Tanzania TRA kuondoa vikwazo vya kufanya biashara  vilivyokuwa vinawakabili ikiwemo kubabikiziwa makadilio ya juu ya kodi na baadhi ya watumishi  wasio waadilifu.

Wamesema tangu walipofanya mgomo kwa kufunga maduka wakiomba watumishi wa mamlaka ya TRA kubadilishwa ikitokana na kubambikiziwa makadilio ya juu ya kulipa kodi, kwa sasa mamlaka imewasikiliza na kutatua kero na sasa kwamba biashara zinafanyika kwa uhuru.

Sauti za wafanyabiashara

Kwa upande wake Meneja wa mamlaka ya mapato mkoa wa Kigoma Gabriel Mwangosi amewataka wafanyabiashara  kuweka kumbukumbu sahihi za biashara ambazo zitaepusha wao kubugudhiwa na mamlaka hiyo na kulipa kodi kwa wakati.

Sauti ya meneja wa mamlaka ya mapato kigoma