Uvinza Fm

Michango katika shule za msingi na sekondari ni hiari

07/06/2021, 5:14 pm

Na,Mwanaid Suleiman

Serikali imesema uchangiaji wa michango katika  shule za msingi na sekondari ni wa hiari na  hauusishwi kwa wanafunzi kuzuia masomo yao ikiwa hajalipa michango hiyo

Naibu waziri TAMISEMI

Hayo yamejiri leo bungeni jijini Dodoma wakati Naibu waziri wa TAMISEMI mh David Silinde alipokua akijibu swali la mbunge wa Nkasi kaskazini Haida Joseph Kenani lililohoji kwanini wazazi wanachangishwa michango ya kuchangia elimu kwa shule ya msingi na sekondari wakati serikali imesema  elimu ni bure

Sauti ya naibu waziri wa TAMISEMI

Hata hivyo waziri wa elimu  sayansi na teknologia professa Joyce Ndalichako ameongezea kwa kutoa  wito kwa wazazi kuendelea kutoa ushirikiano na serikali ili watoto waweze kupata elimu bora

Sauti ya Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojia na ufundi

Aidha mh David silinde amehitimisha kwa kusema  serikali inatakiwa kufanya tathimini upya ili kuboresha sera ya elimu na elimu kwa ujumla.