Wakazi wa Matendo watembea umbali mrefu kufuata maji
4 June 2021, 7:51 pm
Na,Glory Paschal
Wananchi wa Kijiji cha Pamila Kata ya Matendo Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, Wameiomba Serikali kuwasaidia kupeleka huduma ya maji kwani wanalazimika kutembea umbali mrefu kutafuta maji na kushindwa kufanya shughuli za maendeleo
Wakizungumza na Radio Uvinza Fm, Wananchi hao wamesema kwa muda mrefu wamekuwa wakitumia maji ya visima jambo ambalo linasababisha kuendelea kusumbuliwa na magonjwa ya mlipuko
Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Pamila Adam Senga na Rulai Bakari mwanyekiti wa Kitongoji hicho wamesema tatizo la maji katika kijiji hicho limedumu kwa takribani zaidi ya miaka 15 na wananchi hulazimika kutumia maji yaliyotuwama
Naye diwani wa Kata ya Matendo Issa Ramadhani amesema tayari kata hiyo imetengewa fedha ambayo itatumika kufikisha huduma ya maji katika kata hiyo
Kwa Upande wake Meneja wa Mamlaka ya maji Safi na Usafi wa Mazingira vijijini Ruwasa Halmashauri ya Wilaya Kigoma Respisius Mwombeki amekiri Kijiji cha Pamila kukaa kwa muda mrefu bila huduma ya maji