Tumbatu FM

Toweni msada wa kisheria ili muondoshe migogoro.

9 March 2026, 2:14 pm

Picha ya wasaidizi wa sheria wa wilaya ya Kaskazini “B” wakiwa katika mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya masuala ya haki za binadamu utawala bora na ukatili wa kijinsia (Picha na Vuai Juma)

“Ikiwa mtawasaidia wananchi kuelewa masuala ya kisheria wataweza kufahamu haki na wajibu wao jambo ambalo litachochoe kupunguza malalamiko wakati wa kufuatilia kesi zao”

Na Vuai Juma.

Wasaidizi wa sheria nchini wamehimizwa kuwasaidia wananchi katika masuala ya sheria ili kuondoa mapungufu yaliyomo ndani ya migogoro inayohitaji msada wa kisheria.

Wito huo umetolewa na Afisa tathimini na ufuatiliaji Idara ya maendeleo kanisa katolik Zanzibar Msafiri Thomas Mombo  wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya masuala ya haki za binadamu ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa uwezeshaji wa jamii kwa ajili ya haki za binadamu na utawala bora unaosimamiwa na shirika la maendeleo la kanisa katoliki yaliyofanyika kwenye kituo cha utegemeo Welezo Mkoa wa Mjini Magharib.

 Amaesema  chimbuko la mradi huo nikutokana na tathimini ambayo wameifanya  mnamo mwezi March 2025 iliyoonesha kuwepo kwa upungufu wa namna ya matumizi na uelewa wa sheria na kufikia msada kwa haraka  na kugundua  ushirikishwaji mdogo wa masualaya maamuzi ndani ya jamii hasa kwa makundi ya wanawake na vijana.  

Sauti namba 1 ya afisa tathimini na ufuatiliaji Idara ya maendeleo kanisa katolik Jimbo la Zanzibar Msafiri Thomas Mombo.

Amesema wameandaa mbinu mbali mbali ili kuweza kufikia mipango yao ikiwemo uundwaji wa kamati zitakazo fuatilia wanajamii wanaokumbana na changamoto za kisheria ndani ya shehia zinazonufaika na mradi huo Pamoja na kuwawezesha wasaidizi wa sheria kuweza kuwafikia vijana huku akisema wamepanga kuwafikia walengwa wapatao 10500 ndani ya shehia hizo.

Ni sauti ya 2 ya afisa tathimini na ufuatiliaji Idara ya maendeleo kanisa katolik jimbo la Zanzibar Msafiri Thomas Mombo akiwa kwenye kikao na wasaidizi wa sheria.

Hata hivyo amesema katika utekelezaji wa mradi huo matarajio yao ni kuiona jamii kuwa na uwezo wa kufikia mijadala ya kimaamuzi na kupata uwezo wa kufikia kiwango cha kudai haki zao.

Ni afisa tathimini na ufuatiliaji Idara ya maendeleo kanisa katolik jimbo la Zanzibar Msafiri Thomas Mombo akielezea matarajio yao kwenye mradi wa masuala ya haki za binadamu.
Picha ya mwanasheria  anaesimamia mradi wa haki za bina damu na utawala bora kutoka ofisi ya maendeleo jimbo katoliki la Zanzibar Peter Maswi Marwa(Picha na Vuai Juma)

Kwa upande mwengine  mwanasheria  wa mradi kutoka ofisi ya maendeleo jimbo katoliki la Zanzibar Peter Maswi Marwa  amesema wasaidizi wa sheria wanawajibu wa kuyafahamu majukumu yao wakati wanapofanya kazi zao huku akisisitiza kuwa bado wanajukumu la kusikiliza kero za wananchi na kuwapa usaidizi wa kisheria huku akiwataka kuzingatia mafunzo waliyopatiwa na kuyafikisha kwa wengine.

Ni sauti ya mwanasheria  wa mradi kutoka ofisi ya maendeleo jimbo katoliki la Zanzibar Peter Maswi Marwa.
Ni picha ya Dokta Sikujua Omar Hamdani ambaye ni mkufunzi wa mafunzo ya wasaidizi wa sheria huko Welezo Mkoa wa Mjini Magharib( Picha na Vuai juma)

Kwaupande wake mkufunzi wa mafunzo hayo Dokta Sikujua Omar Hamdani amaesema kutokana na uelewa mdogo wa masuala ya kisheria ndani ya jamii wasaidizi wa sheria wanajukumu la Kwenda  kuibua na  kutoa elimu ya msada wa kisheria ili vitendo vya udhalilishaji viweze kupungua.

Sauti ya mkufunzi wa mafunzo ya masuala ya haki za binadamu na utawala bora Dokta Sikujua Omar Hamdani.

Nao washiriki wa mafunzo hayo wamesema elimu waliyopatiwa itakwenda kuwasaidia sana wakati watakaporudi kwenye jamii yao huku wakikiri kuwepo kwa matukio mabaya ikiwemo ukatili pamoja na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Ni sauti za washiriki wa mafunzo waliopata nafasi ya kuzungumza.