Tumbatu FM
Tumbatu FM
21 February 2026, 9:36 am

” Tumetoa sadaka ya ftari kwa watu wapatao 500 lengo ni kusaidia watu wenye hali ngumu na huu ni utaratibu wetu ambao huwa tunaufanya kila baada ya muda hata ikiwa sio wakati wa mfungo wa mwezi wa Ramadhani”
Na Juma Haji.
Taasisi ya Sister Island imeendeleza utaratibu wake wa kugawa ftari kwa wazee wa wanafunzi wa skuli hiyo ambao hufanyika kila ufikapo mwezi mtukufu wa ramadhan.
Akizunguza na waandishi wa habari mara baada ya kukamilika zoezi la ugawaji wa ftari hiyo lililofanyika Nungwi mkoa wa kaskazini Unguja Msimamizi Mkuu wa taasisi hiyo Haji Mohd Ali amesema hadi kukamilika kwa zoezi hilo zaidi ya watu 500 wakaazi wa Nungwi na vijiji jirani wamepatiwa vyakula hivyo.
Amesema katika zoezi hilo vyakula vililivyotolewa ni pamoja na mchele kilo 2,500 na njugu mawe kilo 1,500
Mmoja kati ya watendaji wa taasisi hiyo bibi Sikujua Makame Sua akizungumzia maendeleo ya wanafunzi kwa wazee waliojitokeza kupokea sadaka hiyo amewataka wazazi kujenga tabia ya kufatilia maendeleo ya Watoto wao ili kubaini changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi kwa kushirkianana walimu.
Nae Mkurugenzi wa Taasisi ya Sister Island, Francesca Michael, Ameeleza kuwa utoaji wa sadaka hiyo ni muendelezo wa juhudi za taasisi yake katika kusaidia jamii na kuunga mkono mipango ya serekali kwa wananchi.
Amesema huo ni utaratibu wa kawaida wa taasisi yake ambao hufanyika kila unapofika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani sambamba na kuendelea kusaidia jamii hata katika miezi mingine.
Kwa upande wao, baadhi ya wananchi wa Nungwi wamesema taasisi hiyo imekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya eneo hilo, na imekuwa ikiongeza kasi ya ufaulu kwa wanafunzi.