Tumbatu FM
Tumbatu FM
11 August 2025, 9:46 am

“Ikwa tutashirikiana kwa pamoja katika kuwasimamia watoto wetu tutaweza kuongeza idadi ya ufaulu ndani ya Skuli yetu”
Na Atka Mosi.
Mwalim Mkuu wa skuli ya sekondari Mkokotoni Haji Abdallah Seif amewataka wazazi na walezi kutoa mashirikiano kwa kuwasimamia watoto kupata haki yao ya elimu ili kuongeza idadi kubwa ya ufaulu.
Akizungumza na Tumbatu Fm huko ofisini kwake Mkokotoni amesema kujengwa kwa skuli hiyo kutasaidia ongezeko la ufaulu kwa wanafuzi na kuondokana na changamoto ya kufuata elimu masafa ya mbali jambo ambalo lilikua linawapa ugumu wazazi kuwapeleka watoto wao katika skuli za mbali.
Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeboresha miundombinu mbali mbali ikiwemo ya elimu kwa wananchi wake ili kuongeza wataalamu katika nchi huku akitoa wito kwa serikal kuwatatulia changamoto inayowakabili ya kukosa walimu wa masomola sayansi.
Kwa upandewao wazazi wa wanafunzi wanaosoma skulini hapo wamesema wanajivunia maendeleo yaliyofanywa rais wa Zanzibar dkt Hussein Ali Mwinyi ikiwemo kuwajengea skuli ya gorofa iliopo karibu na maeneo yao hali ambayo imewapa faraja huku wakisema kujengwa kwa skuli hiyo maeneo ya karibu kutawaepusha watoto kufanyiwa vitendo viovu ikiwemo udhalilishaji.

“Tunakabiliwa na changamoto nyingi sisi wanafunzi ikiwemo uhaba wa vifaa vya kujifundishia hasa masomo ya sayansi, uhaba wa walimu wa masomo hayo lakini pia hatuna sehemu ya kulala wanafunzi tunajikuta tunalala kwenye vyumba vya madarasa hali ambayo siyo salama kwetu tunaiomba serikali yetu ambayo ni sikivu kututatulia changamoto hizi”
Nao wanafunzi wa Skuli ya Sekondari Mkokotoni wamesema wamefarijika na uwepo wa skuli hiyo mpya ya gorofa na kuahidi kuitunza skuli hiyo huku wakisema wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ambazo zinawarudisha nyuma katika masomo na kuiomba serikali kuwatatulia changamoto hizo zinazowakabili skulini hapo ikiwemo kutokuwepo kwa Dahalia, vifaa vya masomo ya sayani na uhaba wa walimu ili kuweza kufikia malengo waliyo kusudia.