Tumbatu FM

Wapelekeni watoto shule na madrasa mapema kwenda kujifunza

13 July 2025, 4:24 pm

Pichani ni Mwalimu Abdalla Khamis Ali na wanafunzi wa shule ya msingi ya Sister Island iliyopo Nungwi Kiungani, Wilaya ya kaskazini “A” Unguja Picha na Juma Haji.

ikiwa wanajamii watahamasika kuwapeleka watoto wao kwenye vituo vya elimu wakiwa na umri mdogo kutapelekea wanafunzi kuwa na muamko wa masomo yao

Na Juma Haji.

Wazazi na walezi nchini wametakiwa kuwapeleka shule na madrasa watoto wakiwa wadogo ili kupata msingi imara wa elimu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti  bi Mwajuma Haji Mussa na bi Sikujua Makame Sua, ambao ni wazazi wa watoto wanaosoma shule ya Msingi ya Sister Island wamesema watoto wanapopelekwa shule na madrasa mapema hukosa muda wa kuzurura ovyo mitaani na kuepuka kufanya matendo yaliyo nje ya wakati wao.

Wakifafanua zaidi wamesema matukio  ya kutowapatia fursa za elimu watoto mapema hutokea kwa wazazi wenye tamaa ambao huwachukua vijana hao kwenda kuwa wasaidia kazi kwenye biashara zao  ikiwemo  maduka ya mama ntilie pamoja na kubeba ndoo za dagaa.

Sauti za wazazi wa wanafunzi wa shule ya Sister Island kutoka Nungwi Wilaya ya kaskazini “A” Unguja.

Akitoa historia fupi ya maendeleo ya shule ya Sister Island Mwalimu Mkuu msaidizi Khamis Anasi Simai amesema shule hiyo iliyoazishwa mwaka 2019 ikiwa na darasa moja la maandaimepiga hatua kimaendeleo ambapo imeanza kwa madarasa mawili ya msingi na kuongezeka hadi kufikia madarasa sita mwaka 2025.

Sauti ya Mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya Sister Island Khamis Anasi Simaai.