Tumbatu FM

Mikakati ya kulinda amani Mkoa wa kaskazini Unguja yaanza kutekelezwa

4 July 2025, 5:22 pm

Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa kaskazini Unguja Matar Zahoro Masoud akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari kwenye kikao chake cha kila mwezi (Picha na Abdul Sakaza)

Serekali ya Mkoa kwa kushirikiana na vyomb vya ulinzi na usalama tutahakikisha lengo la kutokomeza vitendo viovu linafikiwa

Na Mwanahawa Hassan Khamis

Mkuu wa Mkoa wa kaskazani  Unguja Mh: Mattar Zahor Masoud amesema Ofisi yake imejipanga kuweka mipango madhubuti ya kutokomeza vitend viovu vinajitokeza katika Mkoa huo.

Akizungumza  na waandishi wa Habari Ofisini kwake Mkokotoni amesema Mkoa wa kaskazini Unguja umekuwa na matukio mbali mbali ya uhalifu ikiwemo wizi wa mazoa madawa ya kulevya na vitendo vya uhalifu jambo ambalo linaleta athari katika jamii.

Amesema serekali katika mkakati wake wa kubaini vitendo hivyo itafanya Doria kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama na kuwachukulia hatua wale wote watakaokamatwa.

Aidha akielezea suala la uchaguzi Mkuu Matter amesema serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imejipanga kuimarisha usalama wa raia kwa kutekeleza misingi ya demokrasia itakayomuwezesha kila mwenye sifa ya kusiriki uchaguzi aweze kuifikia haki yake hiyo  ya kikatiba.

Amewataka wadau wa siasa waliopo Mkoa wa kaskazini Unguja kufuata sharia na kanuni pamoja na miongozo yake kwa kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu.

Hata hivyo ametoa wito kwa jamii kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika kupambana na vitendo viovu kwa kuviripoto sehemu husika Ili kuongeza nguvu juhud za serekali katika kupamban na vitendo hivyo.