Tumbatu FM
Tumbatu FM
28 June 2025, 2:13 pm

“Imebainika kuwa kutokuwepo kwa mafunzo ya ndoa kwa vijana kunapelekea kuongezeka kwa talaka zisizo tarajiwa”
Na Vuai Juma.
Jamii imeshauriwa kuisoma na kuifaham ndoa ili kuepukana na wimbi la talaka za kiholela.
Ushauri huo umetolewa na katibu tawala wilaya ndogo Tumbatu Khatib Habib Ali wakati akifungua mafunzo yanayohusu elimu ya ndoa kwa walimu wanaotarajiwa kufundisha masomo hayo yaliyo andaliwa na Jumuia ya Nataraji Social Devlopment Foundation huko ukumbi wa mikutano wa Family Kaba uliopo kisiwani Tumbatu.
Amesema watu wengi ambao wanaingia katika ndoa hawana elimu ya kutosha jambo linalopelekea kuongezeka kwa talaka jambo linalopelekea kuongeza ugumu wa maisha pamoja na watoto kujiingiza katika makundi maovu ikiwemu utumiaji wa dawa za kulevya na ujambazi hali inayosababishwa na ukosefu wa malezi bora.
Kwaupande wake mwenyekiti wa Jumuia ya Nataraji Social Devlopment Foundation Sidiki Juma Khamis amesema kulingana na utafiti ambao wameufanya wamegundua kuwa jamii inakabiliwa na changamoto ya ongozeko la talaka uporomojaki wa maadili na ndoa zisizo na uhakika jambo ambalo limewapelekea kutoa mafunzo kwa walimu hao na kuyapeleka kwenye ili jamii makundi ya vijana.

Tutayatumia mafunzo haya kama inavyo takiwa kwa kuyapeleka kwa wanajamii ili kutatua migogoro ya ndoa.
Kwaupande wao washiriki wa mafunzo hayo wamesema wanaishukuru jumuiya hiyo kwa kuwapa elimu ambayo itakwenda kuwasaidia wao binafsi Pamoja na watu wengine.