Tumbatu FM
Tumbatu FM
11 June 2025, 10:48 am

picha ya wandishi wa habari pamoja na mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja Matar Zahoro Masoud (aliepo mbele) wakiwa kwenye kikao cha pamoja.
Picha na Vuai Juma.
“Iwapo wandishi wa habari watapata mashirikiano kutoka kwa watendaji kutasaidia kujua changamoto zinazowakabili wananchi wetu”
Na Abdul Sakaza.
Mkuu wa Mkoa wa kaskazini unguja Matari Zahor Masoud amekutana na waanishi wa habari ofisini kwake mkokotoni kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na wandishi wa habari na wananchi wa mkoa huo .
Akizungumza katka kikao cha pamoja na wandishi wa habari Matar amesema kuwa serikali inathamini mchango wa vyombo vya habari katika kuhamasisha jamii na kufikisha taarifa sahihi kuhusu shughuli za maendeleo zinazofanywa na serekali.
Amesema mashirikiano na waandishi wa habari ni jambo lisiloepukika kwani waandishi wa habari ndio daraja la kuwaunganisha wananchi na serekali kwa ujumla.
Katika mkutano huo pia amegusia changamoto ya migogoro ya ardhi inayozidi kushamiri katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo akieleza kuwa tatizo hilo linachangiwa kwa kiasi kikubwa na maeneo mengi kutopimwa rasmi na kusema sasa wanapanga mikakati ya kutatua changamoto hizo .
Mhe. Matar amesisitiza kuwa serikali ya mkoa huo itaendelea kusimamia kikamilifu utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kushirikiana na wandishi wa habari wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo huku sambamba na kuwahimiza Wananchi kujitokeza kuvutumia vyombo vya habari kueleza changamoto zao.
kwa upande wao waandishi wa habari wameishukuru ofisi hiyo kwa kuonyesha nia thabiti ya kushirikiana na vyombo vya habari katika kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi na kwa wakati.