Tumbatu FM
Tumbatu FM
4 May 2025, 3:35 pm

Picha ya kamati ya wataalamu wa masuala ya habari Zanzibar (ZAMECO)
Na Vuai Juma
“Uwepo wa sheria kandamizi kwa wandishi wa habari imekua ni changamoto kubwa kwenye utendaji wao wa kazi”
Na Vuai Juma
Mamlaka zinazosimamia sekta ya habari hapa nchini zimetakiwa kuharakisha mchakato wa upatikanaji wa sheria mpya ya habari ambayo itakua Rafiki kwa wandishi wa habari wakati wa kutekeleza majukumu yao.
Wito huo umetolewa na Kamati ya wataalamu wa masuala ya habari Zanzibar ZAMECO pamoja na wadau wa sekta ya habari wakati wakiungana na mataifa mbali mbali ulimwenguni kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani inayo adhimishwa kila ifikapo Mei 3 ya kila mwaka.
Wamesema kwa sasa wandishi wa habari wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikwepo kutokuwepo kwa sheria inayowapa uhuru wa kutekeleza majukumu yao ulinzi wakati wa uchaguzi pamoja na kuripoti bila kubaguliwa hali inayopelekea kuwakosesha wananchi kupata taarifa.
Aidha ZAMECO imewataka wanahabari kutumia kalam zao katika kuvishawishi vyombo vinavyo simamia tasnia ya habari kuijadili na kuipitisha sheria mpya ya habari ili kuleta maendeleo katika sekta hiyo.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu mwaka huu ni sheria nzuri ya habari ni chachu ya uchaguzi ulio huru na wa haki.