Tumbatu FM

Watumishi tumieni ujuzi kuleta mabadiliko

26 December 2024, 10:58 am

Picha ya mstahiki mea wa manispaa ya kaskazini “A” akiwa pamoja na watumishi wa wilaya hiyo katika hafla ya kuwaaga watendaji waliomaliza muda wao wa utumishi.

Picha na Juma Haji.

“ikiwa watumishi watatumia vyema ujuzi walio nao wataweza kutekeleza majukumu yao ya kikazi kwa ufanisi mkubwa”

Na Juma Hai.

Watumishi wa Wilaya Kaskazini “A” Mkoa wa Kaskazini Unguja wamtakiwa kuzitumia vyema taaluma zinazoachwa na wastaafu wa ofisi hiyo ili kuendelea kutoa huduma bora na kwa ufanisi zaidi.

Wito huo umetolewa na mstahiki meya wa Baraza la Manispaa Wilaya Kaskazini “A” Machano Fadhil Babla alipokua akizungumza na Wafanyakazi kutoka ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya kaskazini “A” katika Sherehe za kuwaaga Wastahafu. wa ofisi hiyo.

Amesema ni vyema kwa watendaji kufuata yale yote mazuri ya kitaaluma na kuacha kufanya kazi kwa mazoea hali amabayo itasaidia kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa jamii.

Aidha Mstahiki Meya amesemakuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuwajali wastaafu wake imeweza kuwawekea Mafao Maalum ya kipindi cha ustahafu hii ni kuonyesha kujali juhudi zao katika kipindi chote utumishi wao kwa kuwahudumia wananchi pamoja na kusaidia kukuza Maendeleo ya nchi.

Kwa upande wao Wastahafu hao wameishukuru ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa kuwajali katika muda wote wa utumishi wao pamoja na kuwataka Wafanyakazi kuendelea kuwa na ushirikiano wa karibu katika utendaji wao wa kazi.

Jumla ya wastaafu wanne wameagwa watatu kutoka kitengo cha afisi ya Elimu na mmoja kutoka kitengo cha Usafi afisi ya Mkuu wa Wilaya.