Wananchi watakiwa kuchangia upatikanaji wa maendeleo
25 December 2024, 12:57 pm
Picha ya waziri wa kilimo mifugo na uvuvi Shamata Shame Khamis (aliekamata mkasi) akiwa katika shuhuli ya uwekaji wa jiwe la msingi kituo cha zima moto huko kiwengwa mkoa wa kaskazini unguja.
Picha na Atka Mosi.
“Ikiwa wananchi wataiunga mkono serekali itarahisisha kuchochea maendeleo”
Na Atka Mosi.
Waziri wa kilimo mifugo maliasil zanzibar Shamata shaame khamis amesema juhudi za kuleta maendeleo sijukumu la serikal pekee bali ni jukumu la wananchi wote .
Ameyasema hayo mara baada ya uwekwaji wa jiwe la msingi katika kituo cha zima moto kilichopo kiwengwa wilaya ya kaskazin “B” mkoa wa kaskazin unguja ambapo amewataka maafsa na wapiganaji wa jeshi hilo kusimamia na kuituza miundombinu hiyo kwa kizazi cha leo na taifa kwa ujumla.
Amesema wananchi wengi wanajiisahau kwenye suala la kushirikiana na serekali kupeleka maendeleo katika maeneo yao jambo linalowafanya kuibebesha mzigo mkubwa serekali.
Aidha ameitaka jamii kutoa mashirikiano kwa serekali ili kazi ya kujenga miradi ya maendeleo iwe rahisi.
Hata hivyo amesema kujengwa jengo la kikosi hicho maeneo ya kiwengwa ni kuharakati za kupeleka maendeleo kwa wakaazi wa maeneo hayo hivyo ni vyema maafsa hao kuwajibika kwa wakati pindi ikitokea hitilafu.
Nae katibu mkuu wa ofisi ya raisi tawala za mikoa Issa Mahfudhi Haji amesema kukamilika kwa mradi huo ni utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduz 2020 -2025 ikiwa na lengo la kuimarisha huduma za uwokozi kwa wananchi pamoja na kuboresha mazingira ya kazi kwa wapiganaji wa zima moto.
Nae kamishna wa kikosi cha zima moto na uokozi Zanzibar amewashukuru maafisa wa jeshi hilo kwa kujitoa kwa nguvu zao katika kusimamia mradi na kutoa mafundi na vibarua wao na kutanua mahusiano na mataifa mbali mbali ikiwemo Angola,falme za kiarabu na Iraqi kwa lengo la kuwasaidia vijana katika kuwapatia mafuzo ya uwokozi,