Tutetee haki za watoto tuwalinde na ukiukwaji wa haki za binadamu
13 July 2024, 8:19 am
Ni wajibu wa jamii kuwapa watoto haki zao kwa maendeleo ya baadaye.
Na Abdul Sakaza.
Msimamizi Mkuu Kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) hapa Zanzibar Bi. Laxmi, amewataka vijana Zanzibar kuendelea kutetea haki za watoto ili kuwalinda na ukiukaji wa haki za kibinadamu.
Ameyasema hayo wakati akifungua semina ya siku moja kwa taasisi mbalimbali za Zanzibar iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ONE UN Board room, jengo la ZSTC Kinazini mjini Unguja.
Bi Laxmi amesema vijana wa Zanzibar wana haki na wajibu wa kuzilinda na kuzitetea haki za watoto wa Zanzibar ili waishi katika misingi iliyo bora na ya kujiamini katika jamii.
Aidha ameishauri SerIkali ya Mapinduzi ya Zanzibar kushirikiana na vijana katika kubadilisha sheria na sera zinazomkandamiza mtoto wa Zanzibar ili kuondoa utata kwa baadhi ya sheria.