Ruangwa FM

DC Ngoma apiga marufuku wazazi kuwasubiri watoto maeneo ya shule na kuwapigisha P. A

5 September 2024, 5:47 pm

Na loveness Daniely
Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Hassan Ngoma amepiga marufuku wazazi wenye watoto wanaomaliza darasa la saba wenye tabia ya kuwasubiria viwanja vya shuleni kwa lengo la kuwalaki na kuwazungusha mitaani kwa kutumia bodaboda,bajaji,nk

Marufuku hayo yametokana na madhara ya mara kwa mara kama ajali na watoto kutofanya vizuri katika masomo ya mwisho ya siku za mitihani huku wananchi wakisema ni desturi zao walizo zoea.

Akizungumza na Ruangwa Fm leo Afisa elimu taaluma Abdul Nangomwa wilaya ya Ruangwa amesema mika miwili mfululizo wazazi wamekua wakilalamikia masomo ya mwisho siku za mitihani kutofanya vizuri.

Aidha Nangomwa amewaomba wazazi kuachana na hizo desturi kwani zinawafanya watoto kua na pressure ya kumaliza ili kuona wazazi waliowafuata hapo shuleni hivyo wazazi wawasibri watoto nyumban ili wawalaki huko.

Hata hivyo amesema mpaka sasa maandalizi ya mitihani ya darasa la saba wilaya imejiandaa vizuri nakusihi wazazi kuwaanda watoto kiakili ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao.