Ruangwa FM
Ruangwa FM
19 September 2025, 9:39 pm

Na Loveness Daniel.
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wilaya ya Ruangwa limeanza rasmi utekelezaji wa mradi mkubwa wa laini ya umeme wa msongo wa kilovoti 33 (KV 33), kutoka mjini Ruangwa kuelekea kijiji cha Namungo kupitia Chingumbwa – eneo muhimu la uwekezaji wa shughuli za uchimbaji madini.

Akizungumza katika hafla ya upokeaji wa nguzo za zege zilizowasili leo katika kijiji cha Namungo, Manager wa TANESCO wilayani Ruangwa, Mhandisi Hassan Mustapha, alisema kuwa mradi huu wa zaidi ya kilomita 30 ni hatua kubwa ya kimkakati kwa ajili ya kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika, wenye nguvu na wa kutegemewa kwa wawekezaji wa sekta ya madini.
Kwa upande wake, Filbert Masawe, Meneja wa Kampuni ya uchimbaji madini ya Elianje Genesis Ltd, amesema kuwa mradi huu utatoa fursa kwa wawekezaji kuleta mitambo mikubwa zaidi na kuongeza uzalishaji kwa ufanisiakibainisha kuwa awali tulikua tunatumia umeme wa kiwango cha chini ambao haukuweza kuendesha mitambo mikubwa ipasavyo lakin kupitia KV 33, amesema wanategemea ufanisi na tija kubwa zaidi.

Aidha mwenyekiti wa wachimbaji wa madini katika Mgodi wa Namungo ndg.Francis Mwingira ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Raisi Dkt. Samia Hassan kwa kupitia Tume ya madini na Tanesco kuwezesha mradi huo ambao utaenda kuboresha umeme katika mitambo ya wachimbaji.
Hata hivyo baadhi ya wananchi na wakazi wa Namungo akiwemo Agness Kimath na Edson Tibaijuka wamesema kwa sasa uhakika wa kipato kwa wakazi wa namungo kwa kupitia umeme Unaenda kuimarika huku mama lishe wakifurahia Matumizi ya uhakika wa nishati safi ya umeme kwa kupata umeme wenye Nguvu.