Ruangwa FM

Tuanzie Nyumbani Kuleta Tumaini Jipya kwa Elimu Vijijini Ruangwa

18 August 2025, 11:50 pm

Ruangwa, Lindi 

Katika harakati za kuhakikisha watoto wa vijijini wanapata haki yao ya msingi ya elimu, Umoja wa Wadau wa Elimu Wilaya ya Ruangwa (UWERU) imeanza rasmi kuitekeleza kampeni ya “Tuanzie Nyumbani” yenye lengo la kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa elimu na kupinga vitendo vya ukatili kwa watoto, ikiwa kampeni hiyo imeanzia leo katika shule ya msingi Nanjaru pamoja na kufanyika mkutano uliohushisha wazazi.

Kampeni hiyo, inayoendeshwa kwa ushirikiano kati ya Halmashauri ya Wilaya, mashirika yasiyo ya kiserikali, viongozi wa dini, na wazazi, ambayo imeanza leo 18 August 2025 katiaka kijiji cha Nanjaru kata ya Nambilanje inalenga kufika kijiji kwa kijiji kuhamasisha wananchi kuchukua hatua madhubuti dhidi ya changamoto zinazowakumba watoto kielimu.

Akizungumza na wanafunzi Shule ya msingi Nanjaru ,Afisa Mradi kutoka Hope 4 Young Girls, Bi Latfa Waziri Kijazi alisema Mradi huu umebeba maono ya kutoa elimu, kuhamasisha, na kufuatilia changamoto za watoto shuleni ili kupunguza kiwango cha wanaoacha masomo.

Huku akiwakumbusha wanafunzi namna ya kujipambanua ili kutimiza malengo yao ya kielimu.

sauti ya Afsa miradi Bi Latfa Kijazi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa AKUVIKIRU Ruangwa, Bw. Abdul Mitumba alieleza kuwa utoro na kuacha shule ni changamoto kubwa hasa katika maeneo ya vijijini, ambako mazingira duni na mtazamo wa baadhi ya wazazi kuhusu elimu bado ni tatizo.

sauti ya Abdul Mitimba AKUVIKIRU

Eddo Mbaruku kutoka SMAUJATA Ruangwa aliongeza kuwa ukatili wa kijinsia umeendelea kuwa chanzo kikuu cha watoto hasa wa kike kukatiza masomo. Alisisitiza kuwa ulinzi wa haki za watoto unapaswa kuwa ajenda ya kila mzazi na kiongozi wa kijamii.

Edward Mbaruku akielimisha wanafunzi S/M Nanjaru kuhusu Ukatili.

Katika mkutano huo, baadhi ya wazazi walikiri kuwa uelewa mdogo juu ya umuhimu wa elimu na changamoto za kiuchumi zimekuwa kikwazo, lakini walieleza utayari wao wa kushirikiana na wadau kuhakikisha watoto wao wanapata elimu bora hukuwakifikisha kero zao kwa serikali.

sauti ya mzazi

“Tuanzie Nyumbani” ni kampeni ya elimu iliyoanzishwa na Hope 4 young grils ,Umoja wa Wadau wa Elimu Ruangwa kwa ushirikiano na serikali, taasisi zisizo za kiserikali, na wadau mbalimbali ikiwa na Malengo  yaKuongeza uelewa juu ya haki ya mtoto kupata elimu,Kupambana na utoro mashuleni,Kupinga ukatili dhidi ya watoto na Kuhamasisha ushiriki wa jamii katika malezi ya kielimu.