Ruangwa FM
Ruangwa FM
13 June 2025, 8:22 pm

Na loveness josefu
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (MB), anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe ya kufunga Maonesho ya Madini na Fursa za Uwekezaji Mkoa wa Lindi (Lindi Mining Expo 2025)
Taarifa hiyo imethibitishwa leo 13Jun 2925 na Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea mabanda ya maonesho hayo yaliyoanza tarehe 11 Juni 2025.
“Nimeridhishwa sana na maandalizi. Naipongeza kamati ya maandalizi kwa kazi kubwa na ya kiwango cha juu,” alisema Dkt. Kiruswa.
Ameongeza kuwa hafla ya kufunga itakuwa ya kipekee, akiwakaribisha wananchi na wadau wote kushiriki kwa wingi ili kujifunza na kunufaika na fursa zinazopatikana kupitia sekta ya madini na uwekezaji mkoani Lindi.