Ruangwa FM

Kaliua wasafiri Km. 1,500 kujifunza mfumo wa stakabadhi ghalani Ruangwa

17 December 2024, 11:45 am

Mkuu wa wilaya ya Kaliua Dkt Mongella akizungumza katika mafunzo.

Na loveness Daniel

“Tumetembea km1500 kutoka Kaliua Tabora kuja kujifunza mfumo wa stakabadhi za ghala katika wilaya hii ya ruangwa iliyopga hatua katika mfumo na kuleta tija”amesema DC Mongella

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa wilaya ya ya Kaliua Dkt Gerad Mongella leo 16 Dec2024 wakati wa ziara ya kujifunza mfumo wa stakabadhi ghalani wilayani Hapa

“ Tumekuja kujifunza hapa maana tunapakuanzia kwakua sisi ndo wazalishaji wakubwa wa tumbaku Tanzania kwani tuna amcos 173 tutazitumia hizo kuanzisha mfumo huu kuwa tija katika jamii.”amesema Gerad Mongella

Naye mkurugenzi wa halmashauri ya Kaliua Jerry Mwaga amesema wameshawishika kujifunza mfumo huo baada ya kuona halimashauri ya wilaya ya rungwa inanufaika  na mapato pia mfumo huo kwao utasaidia kujua takwimu ya wakulima kupitia mazao tofauti na halimashauri kukusanya mapato yake na kujiendesha vizuri.

Aidha mwenyekiti wa halimashauri ya wilaya ya Kaliua Mh Japhael Lufungija amebainisha kua mara kadhaa wananchi wa Kaliua wanashindwa kupata manufaa kulingana na uuzaji holela wa mazao kwa madalali kwani wananunua kwakujihiari.

“Kaliua tunalima mazao mchanganyiko ya mpunga,karanga, Mahindi, tutaenda kuyaweka kwenye mfumo nasisi kama viongozi tumeona tuwakilishe wananchi tujifunze na tukatoe elimu kwa wananchi wetu jinsi mfumo unavyoendesha ili tukalete tija kwa wakulima kwakuwa wanauhitaji katika uuzaji wa mazao“amesema Lufungija

Awali akitoa mafunzo Kaimu mkurugenzi halimashauri ya wilaya ya Ruangwa Nolasco Kilumile ambae ni Afisa kilimo amesema mfumo huo hadi kuleta manufaa katika jamii unahusisha Mkulima, Msafirishaji,muendeshaji wa Ghala,amcos, vyama vikuu vya ushirika,Mnunuzi, Taasisi za fedha , pia  Bodi ya zao husika pamoja na mfumo wa TMX ambao ndio unasimamia uuzaji wa mazao kwa sasa Tanzania.

Afsa kilimo Nolasco Kilumile akitoa mafunzo.

Ziara hiyo imehusisha Viongozi mbalimbali kutoka Halimashauri ya wilaya ya Kaliua Akiwemo DC,wakuu wa idara,Madiwani, maafisa ushirika, Mrajisi mkoa wa Tabora, Ambapo wametembelea pia mradi wa uwanja wa majaliwa stadium na Shule ya msingi ya kisasa Likangara.