Ruangwa FM

Mwanafunzi afariki kwa kuangukiwa na kabati Kilwa

21 November 2022, 3:35 pm

Mwanafunzi wa Darasa la kwanza aliejulikana kwa jina la Adam Kaisi Jika (9) katika shule ya msingi Singino, wilayani kilwa mkoani Lindi, amefariki dunia baada ya kuangukiwa na kabati la kuhifadhia vitabu na madaftari wakati akicheza na wenzake shuleni hapo.

Inaelezwa tukio hilo lilitokea Novemba 17,2022 ambapo wakati wa mapumziko, marehemu akiwa na wenzake alikwenda kwenye chumba kinachotumiwa na wanafunzi wa darasa la pili, wakiwa wanacheza walianza kukimbizana ndipo alipoangukiwa na kabati hilo na kusababisha kichwa kugonga sakafuni na kupata jeraha kichwani.

Kwa mujibu wa taarifa ya mwenyekiti wa kitongoji cha Singino Bw. Hemedi Juma, amesema mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi katika zahanati ya kinyonga na jeshi la polisi wilayani humo imeruhusu familia kuendelea na mazishi.