Wananchi Ruangwa walia na kero ya katizo la umeme
16 April 2021, 5:18 pm
Wananchi Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi wamelalamikia tatizo la kukatika umeme mara kwa mara bila taarifa hali inayoelezwa kusababisha kusimama kwa baadhi ya shughuli mbalimbali hasa zile zitegemeazo nishati hiyo muhimu katika jamii.
Baadhi ya wananchi hao hasa kundi la wafanya biashara wadodgo wadogo, wa mabucha, saluni na hata watoa huduma za kutoa kopi wanaotumia mara kwa mara nishati hiyo wamedai limekua tatizo sugu kwa shirika Hilo la umeme Tanzania (TANESCO) tawi la Ruangwa kukata umeme bila taarifa.
Kufuatia uwepo wa hali hiyo kaimu Maneja wa shirika la umeme tawi la Ruangwa, Lameck Njombo amekiri kuwapo kwa tatizo hilo na kueleza sababu zinazopelekea hali hiyo kuwa ni kutokana na uwepo wa miundombinu chakavu na kukosekana kwa uimara wa nguzo za umeme ambapo ameeleza kuwa wanarekebisha nguzo hizo na kwamba kufikia mwezi wa tano mwaka huu watakua wamekamilisha hivyo amewaomba wananchi kuwa wavumilivu kwani huduma hiyo inaboreshwa na hivi punde itaimarika.