Ruangwa FM

Wazee na viongozi wa dini ruangwa watakiwa kuhubiri amani kuelekea uchaguzi mkuu

22 October 2020, 2:08 pm

Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Ruangwa mkoani Lindi FRANK CHONYA amewataka wazee na viongozi wa dini wilayani humo kuhimiza amani na mshiskamano kwa wananchi na familia zao kuelekea uchaguzi mkuu octoba 28 mwaka huu ili Taiafa liweze kuendeleza maedeleo na sio kusuluhisha migogoro itakayotokana na uvunjifu wa amani katika kipindi cha ucjhaguzi.

Chonya aliyasema hayo alhamisi 22/10/2020  alipokuwa anazungumza na viongozi wa dini na wazee maarufu wilayani humo, iliokwenda sambamba na kuwahimiza kujitokeza kupiga kura kwa wale waliojiandikisha na kuwataka wazee hao kuhimiza vijana na wananchi waliojiandikisha wajitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura ili kuchangua viongozi wanao wataka.

nia yetu kubwa ilikuwa ni kuhakikisha elimu ya mpiga kura, amani,utulivu na mshikamano ndivyo vitawalale kuanzia sasa hadi wakati wa kupika kura na baada ya kupiga kura” Alisema CHONYA ambae ni msimamizi wa uchaguzi jimbo la Ruangwa.

Aidha msimamizi huyo wa uchaguzi ametoa onyo wa wote wataojihusisha kuashiria vitendo vya uvunjifu wa amani kuwa seriali haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria kwa watakaobainika .

atakaejichukulia sheria mkononi hatua dhidi yake za kisheria zitachukuliwa bila woga”. Aliongeza Chonya.

Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Ruangwa mkoani Lindi, Frank Chonya, alipokuwa akizungumza na wazee na viongozi wa dini wilayani ruangwa kuhusuu kuhimiza amani kuelekea uchaguzi mkuu octoba 28 mwaka huu.

Kwa upande wa baadhi ya wazee na viongozi wa dini waliohudhuria kikao hicho wakiwamo Juma omari, Gibson Mujuni na Ismail mawata wamehimiza baadhi ya wazazi kukemea vijana wao wenye tabia za kufanya vurugu nyakati za uchaguzi, pamoja na kukemeana miongoni mwao kuhakikisha wanafuata sheria na kanuni kwa mujibu wa tume ya uchaguzi badala ya kusikiliza maneno ya watu wasiohusika ambao mara nyingi wamekua wakipotosha.

wazee wenzangu tukirudi nyumbani tuwakalishe watoto wetu na tuwaeleze ukweli juu ya kuwa na nidhamu katika kipindi hiki cha uchaguzi na kipindi chote ili kuimarisha amani ya nchi jukumu la kuelimisha watoto wetu ni letu wazazi na viongozi wa dini tusilikwepe” alisema  mzee Juma Mangandila.

Jimbo la Ruangwa litajwa kuwa na jumla ya vituo 311 ambavy vitatumika kwa ajili wa kupigia kura siku ya uchaguzi octoba 28 mwaka huu.