DC Ruangwa: Wakulima lindeni mazao yenu
19 October 2020, 10:40 am
Mkuu wa wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi MH. HASHIM MGANDILWA, amewataka wakulima kuwa na utaratibu wa kuzidikiza mazao yao ghala kuu yanapotoka katika vyama vya msingi ili kuepuka ubadhilifu unaofanywa na baadhi ya wasafirishaji wakishirikiana na viongozi wa vyama vya ushirika.
Mgandilwa ameyasema hayo alipokuwa anazungumza na wakulima wa kijiji cha NANDANDALA, ambao wamekua wakilalamikia tuhuma za chama cha ushirika wa mazazo NANAMBU AMCOS kuwa na viongozi wasio wadilifu, ambapo wamekua na mwenendo wa kuwadhulumu wakulima idadi ya kilo za mazao wanayokusanya na wakati mwingine hata malipo kutolipwa kwa uhalali kulingana na idadi ya kilo walizopima.
kufuatia hatua hiyo mkuu huyo wa wilaya ameagiza wakulima hao kuwa na kawaida ya kusindikiza mazao yao wanapopeleka ghala kuu na kuwa si kosa kwa wakulima hao kuchukua uamuzi huo huku akiwataka kuchagua viongozi wenye uadilifu mara inapofika wakati wa uchaguzi wa viongozi wataohudumu katika chama hicho cha ushirika.
Awali baadhi ya wakulima wakiwamo Bi. Eleba Hassan na Saidi Mohamedi walieleza ushuhuda wa waao kuwa miongoni mwa wakulima waliobiwa kilo zao za korosho na ufuta huku wakilalamikia pia kutozwa tozo mbali mbali mbazo hawakuwahi kufahamishwa kabla.
Chama cha ushirika NANAMBU ni miongoni mwa vyama vinavyotajwa kuwa na viongozi wasio waadilifu ambapo wamesababisha hasara kwa wakulima , ambapo kwa msimu wa mazao 2018/2019 walisababisha hasara ya upotevu wa zaidi ya milioni 20, Viongozi ambao baadhi yao wanatajwa kuwa walihusika, walishawajibishwa na wengine kutolewa madarakani.